HABARI ZA UHAMISHO JANUARI: PATA TETESI KUTOKA MAN UNITED, ARSENAL, CHELSEA, LIVERPOOL, BARCA, MADRID N.K.

Habari kuu za uhamisho kutoka Ligi ya Uingereza, La Liga, Serie A na ligi nyingine dirisha la usajili linapoelekea kufungwa Uingereza.


MAN CITY WANAANDAA €56M KUMSAJILI BUSQUETS


Meneja wa Manchester City Pep Guardiola yupo tayari kufanya mchakato wa kumsajili Sergio Busquets kutoka Barcelona, kwa mujibu wa  Don Balon .

MAN UTD YAMWONGEZA KLUIVERT KWENYE ORODHA


Justin Kluivert Ajax

Manchester United wamemwingiza Justin Kluivert kwenye orodha ya wachezaji wanaotaka kuwasajili dirisha la uhamisho wa Januari, kwa mujibu wa  Yahoo Sport .
Kinda huyo wa miaka 18 mtoto wa gwiji la Kidachi Patrick amebakiwa na miezi 18 kwenye mkataba wake, lakini Thomas Lemar, Malcom na Christian Pulisic pia wameingia kwenye rada kwani Jose Mourinho anataka kusajili winga mpya kwenye kikosi chake.

ARSENAL YAPIGANA VIKUMBO NA UNITED KUMSAJILI RUGANI


Daniele Rugani Juventus Barcelona
Arsenal wameingia kwenye mbio za kumsajili beki wa Juventus Daniele Rugani, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Manchester United, the Sun  limeripoti.

REAL YASAKA MNUNUZI WA RONALDO


Cristiano Ronaldo, Real Madrid

Real Madrid ipo tayari kumuuza Cristiano Ronaldo ikiwa itatokea timu yenye dau nono  Diario Gol .
Licha ya kuendelea kuongeza mataji kwenye klabu hiyo ya Hispania, kuna hisia ndani ya Santiago Bernabeu kuwa Mreno huyo nguvu zake zinaanza kufifia.

MAN UTD YAJIPANGA KUMSAJILI PULISIC


Christian Pulisic Borussia Dortmund
Manchester United imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kumwania kiungo wa Borussia Dortmund Christian Pulisic, kwa mujibu wa  Daily Mail .

LEMAR ANAPENDA KWENDA LIVERPOOL


Thomas Lemar MonacoNyota wa Monaco Thomas Lemar anapendelea kwenda Liverpool kuliko Arsenal dirisha la uhamisho wa Januari kwa mujibu wa  The Independent .
Arsenal walishindwa kukamilisha dili la £90 milioni kwa ajili ya Lemar majira ya joto na inaaminika wanajipanga upya kumsajili winga huyo uhamisho wa Januari, Chelsea nao wakionyesha nia kumsajili.

SPURS YAMTENGEA DAU NONO SUAREZ


Luis Suarez Barcelona
Tottenham wanaandaa dau nono kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez, kwa mujibu wa  Don Balon .
Spurs wanaamini Barcelona watakuwa tayari kumuuza Suarez kwani wanalenga kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann, na miamba hao wa London wameshaanza mazungumzona wawakilishi wa mchezaji huyo.
Lakini mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool anasita kuondoka Camp Nou licha ya kuongezeka ushindani wa namba.

MAN UNITED YACHUANA NA REAL KUMPATA HAZARD


Eden Hazard Chelsea
Manchester United wamejipanga kupigana vikumbo na Real Madrid kwa ajiliya saini ya Eden Hazard, kwa mujibu wa  Sun .
Hazard na bosi wa United wamefanya kazi pamoja wakiwa Chelsea, na kufanikiwa kunyanyua taji la Ligi Kuu msimu wa 2014-15.
Na gazeti hilo limedai kuwa United watatoa dau la paundi milioni 90 kwa ajili ya mchezaji huyo msimu ujao. 

PSG YAMFUATILIA DIARRA


Lassana Diarra | Marseille
Paris Saint-Germain wapo kwenye mazungumzo na mchezaji wa zamani wa Chelsea na Real Madrid Lassana Diarra, kwa mujibu wa  SFR Sport 
Diarra kwa sasa anaichezea klabu ya Al Jazira ya Falme za Kiarabu, lakini anaweza kuruhusiwa kuondoka kwa uhamisho wa bure Januari.

NAPOLI YAMFUKUZIA KIUNGO WA CITY


Oleksandr Zinchenko Manchester City
Napoli itaanza upya jitihada za kumsajili kiungo wa Manchester City Oleksandr Zinchenko kwenye dirisha la uhamisho Januari, kwa mujibu wa  TuttoMercatoWeb
Zinchenko alijiunga na City mwaka 2016, lakini msimu uliopita alikuwa akitumika kwa mkopo PSV kabla ya kuivutia Napoli majira ya joto.

ATLETICO KUMUUZA GRIEZMANN KWA MAN UNITED


Antoine Griezmann Atletico Madrid Roma
Atletico Madrid wapo tayari kumuuza Antoine Griezmann kwa Manchester United ili kuepuka kumuuza kwa Barcelona ambao ni wapinzani wao, kwa mujibu wa  Metro .  

MASCHERANO KUTIMKIA CHINA


Javier Mascherano Barcelona
Uhamisho wa Javier Mascherano kwenda Hebei China Fortune ni kama umekamilika baada ya Barcelona kukubali kumwachilia mchezaji huyo, kwa mujibu wa  Marca .
Barcelona wanaweza kupata hadi milioni 10 kwa kumuuza beki huyo ambaye ameanza kukosa nafasi kikosi cha kwanza msimu huu.

ARSENAL INATAKA KUMSAJILI DAVID LUIZ


David Luiz Chelsea
Arsenal wameandaa kitita cha £30milioni kwa ajili ya beki wa Chelsea David Luiz, kwa mujibu wa habari kutoka  Daily Express .
Luiz ameichezea Blues mechi nane tu msimu huu Ligi Kuu Uingereza, baada ya kushindwa kumshawishi Antonio Conte.
Inafahamika kuwa mahusiano yao hayajapona vizuri, na Arsene Wenger sasa anavutiwa kuipata saini ya Mbrazili huyo.
Imeripotiwa kuwa Luiz ni shabaha ya Jose Mourinho na Manchester United, kadhalika Juventus na Real Madrid.

DE BRUYNE MBIONI KUSAINI MKATABA MPYA CITY


Kevin De Bruyne Manchester City
Kevin De Bruyne anakaribia kusaini mkataba mpya wa muda mrefu Manchester City, kwa mujibu wa BBC .
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ameibukia kuwa mmoja wa viungo bora katika ulimwengu wa soka akiiwezesha timu ya Guardiola kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Uingereza kwa pengo la alama 11.

ARTETA APANGWA KUWA MRITHI WA WENGER


Mikel Arteta Arsenal FA Cup Trophy Parade 31052015
Mikel Arteta ndiye anayeweza kupewa mikoba ya Arsenal kumrithi Arsene Wenger, kwa mujibu wa  Daily Telegraph .
The former Spain international is currently working at Manchester City under Pep Guardiola, but is held in high regard by the Gunners.
Wenger's current contract expires in 2019, and Arsenal are working up a shortlist of replacements, with Arteta near the top of the list
Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Hispania kwa sasa anafanya kazi Manchester City chini ya Pep Guardiola, lakini anapewa nafasi kubwa na Gunners.
Mkataba wa Wenger unafikia mwisho 2019 na Arsenal wameanza kuangalia makocha wanaoweza kuwa mbadala wake, Arteta akiwa wa kwanza kwenye orodha.

DORTMUND WANANAMTAKA MKHITARYAN WAO


Henrikh Mkhitaryan, Man Utd
Borussia Dortmund wanaendelea kuonyesha nia ya kumrejesha mshambuliaji wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan kwenye klabu yao, kwa mujibu wa The Independent .
Mkhitaryan aliondoka Dortmund kutua Old Trafford majira ya joto 2016, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Armenia ameshindwa kuleta ushawishi chini ya Jose Mourinho.
Bosi wa United hajakataa uwezekano wa kuuza wachezaji Januari, na kufuatia habari zilizojiri anaweza kumruhusu Mkhitaryan kurejea Bundesliga na kumruhusu Mourinho kumsajili Julian Weigl.

MAN UTD YATENGA £60M KUMSAJILI SANDRO


Alex Sandro Juventus
Manchester United wanajipanga kutoa kitita cha paundi milioni 60 kwa ajili ya beki wa Juventus Alex Sandro uhamisho wa Januari, kwa mujibu wa  Daily Mirror .
Bosi wa United amekuwa akivutiwa na kazi ya Mbrazili huyo mara kadhaa kwani anataka kuimarisha zaidi safu yake ya mabeki Old Trafford.

ARSENAL KULIPA €48M KUMSAJILI LOZANO


Hirving Lozano PSV
Arsenal wapo tayari kutoa €48 milioni kwa ajili ya nyota wa PSV Hirving Lozano, kwa mujibu wa habari kutoka Mexico.
Lozano anacheza Eredivisie msimu wake wa kwanza na ameshafunga magoli 10 na kutoa pasi sita za magoli katika mechi 15 tu msimu huu, akizivutia Gunners na Everton.

DORTMUND YAKARIBIA KUMPATA ROMERO


Maximiliano Romero Tigre Velez Superliga Fecha 1 25082017
Borussia Dortmund inakaribia kumsajili Maximiliano Romero kutoka Velez Sarsfield, Bild  limeripoti.
Mshambuliaji huyo, 18, anaweza kugharimu takribani €12 milioni, na Dortmund wanaamini anaamini atakuwa mrithi sahihi kwa Pierre-Emerick Aubameyang.

WEST HAM WAMTENGEA DAU ARTER


Harry Arter Bournemouth
West Ham wanataka kumsajili Harry Arter kutoka Bournemouth, kwa mujibu wa The Sun .
Bosi wa Wagonga nyundo David Moyes anataka kuimarisha safu yake ya kiungo na anaamini kuwa Arter, ambaye hajapata nafasi kikosi cha kwanza msimu huu ni suluhisho sahihi.

BARCA YAKARIBIA KUMSAJILI KINDA WA ZAMANI WA CITY


Luis Suarez Jordi Alba Barcelona
Barcelona wanakaribia kumsajili kinda nyota wa zamani wa Manchester City Jose Angel Pozo, kwa mujibu wa  Onda Cero .

Comments