Chadema yakanusha Mwanachama wao kujivua uanachama.

Baada ya taarifa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Mbunge wa Kibamba , John Mnyika  amejivua uanachama kwenye chama chake cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),  chama hicho kimekanusha habari hizo kwa kusema kuwa hazina ukweli wowote za zinapaswa kupuuzwa.
Chadema wametoa kanusho hilo kupitiaukurasa wake wa Twitter, kwa kusema wanaosambaza habari za Mnyika kujivua uanachama ni wale walioishiwa hoja na majibu juu ya maisha ya watanzania.

Kuna taarifa zinasambazwa mitandaoni ya kuwa Mhe. @jjmnyika, Mbunge wa Kibamba amejivua uanachama wa CHADEMA.
Taarifa hizo ni za uongo na hazina ukweli wowote, ni za kupuuzwa, wanaozisambaza ni wale walioishiwa hoja na majibu juu ya hali ya maisha ya Watanzania. Umesema ujumbe ulioandikwa Twitter na cham
chanzo: zanzibar24.

Comments