
Alisema Tafiti hizo
zinazopaswa kwenda kitaalamu zaidi zinaweza kusaidia kwa kiwango
kikubwa uimarishaji sambamba na upatikanaji wa huduma za Maji safi na
Salama katika maeneo mbali mbali Mjini na Vijijini Unguja na Pemba.
Balozi Seif Ali Iddi
alitoa ushauri huo wakati akibadilishana mawazo na Uongozi wa Ngazi ya
juu wa Kampuni ya Global Agence Limited kutoka Nchini Uturuki
ukiongozwa na Mwenyekiti wake Bwana Baddal Çalikuşu { baddal chalkusu }
ambao uko Zanzibar kwa ziara ya kuelezea Taaluma iliyokuwa nao Kampuni
hiyo katika kuendesha miradi inayosaidia utatuzi wa huduma za Maji.
Alisema Zanzibar
imebarikiwa kuwa na vianzio vingi vya maji hasa wakati wa Msimu wa
mavua za Masika lakini hatimae rasilmali hiyo huishia Baharini na
mengine kukauka kabisa bila ya matumizi sahihi ya msingi.
Balozi Seif alisema Maji
ya mvua kwa Mataifa yaliyoendelea Kiteknolojia hutumiwa kwa matumizi ya
kawaida ya nyumbani baada ya kufanyiwa mchujo, ujenzi wa Mabwawa
yanayotumika kwa kufugia samaki sambamba na matumizi ya kilimo
mashambani.
Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar alieleza kwamba upo umuhimu wa kuendeleza ushirikiano kati
ya Wataalamu wa Kampuni hiyo ya wale Wazalendo wa Mamlaka na Taasisi za
Maji Nchini ili kuona rasilmaji ya Maji Visiwani Zanzibar inatumiwa
kitaalamu na kwa uangalifu zaidi.
Mapema Meneja wa
Usafirishaji ambae pia ni Mkuu wa Maendeleo ya Biashara wa Taasisi ya
Tarbim iliyo chini ya Kampuni ya Global Agence Limited Bwana Osan Liman
alisema Taasisi yao imekuwa ikifanya Utafiti na kusaidia Taaluma ya
upatikanaji wa huduma za maji safi na salama katika maeneo mbali mbali
Duniani.
Bwana Osman alimueleza
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Wataalamu wa Taasisi hiyo
iliyoasisiwa mnamo Mwaka 1957 hivi sasa wameboreka zaidi Kiteknolojia
kasi iliyosababisha kuendelea kutoa huduma kwa zaidi ya Nchi 50
Duniani.
Alisema kwa sasa
wanaendelea kutafuta mbinu na njia zitakazosaidia kukabiliana na tatizo
la huduma za Maji katika kiwango cha Kisasa kinachokwenda sambamba na
matumizi ya Mita zinazochangia matumizi hayo kwa kiwango na uangalifu
mkubwa.
Bwana Osman alieleza
kwamba mbali ya Sekta ya Maji lakini Kampuni ya Global iliyozaa Taasisi
mbali mbali za Kiufundi imekuwa ikiendesha Miradi ya Kihandisi kwenye
Sekta za Afya, Miundombinu, huduma za Umeme, Habari na Mawasiliano
pamoja na Kilimo.
Kampuni ya Global Agence
Limited kutoka Nchini Uturuki inatoa huduma za Kitaalamu katika Mataifa
tofauti Ulimwenguni yakiwemo yale ya Bara la Afrika kama Angola, Ghana,
Misri, Tunisia, Malawi, Msumbiji, Namibia, Sudan, Mauritania ambapo kwa
sasa pia wapo Bagamoyo Nchini Tanzania kufanya utafiti katika Sekta ya
Maji.
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
29/12/2017.
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
Comments