
Akizungumza katika mahafali ya kwanza kwa wananfunzi Chuo cha ufundi
na Biashara Magomeni (Microtech Institute Of Business and Technology )
yaliyofanyika magomeni amesema Zanzibar ni sehemu yenye uwezo wa
kuzalisha wanafunzi wa zuri ni ni vyema kwa taasisi hizo kuelekeza nguvu
zao katika ujenzi wa vyuo.
Amesema kwa sasa taifa linahitaji wasomi katika kuendeleza maendeleo
ya kiuchumi hivyo ni vyema kwa wananfunzi kuendelea kujifunza katika
katika nchi pamoja na kuwa na utamaduni wa kujiendeleza kitaaluma ili
waweze kufanya kazi zinazoendana na soko la ajira.
Kwa upande Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa
pili Raisi Mihayo Juma N’hunga amewataka wahitimu hao kutumia vyema
ujuzi walioupata katika kutumikia taifa pamoja na kuwa na utamaduni wa
kujiajiri ili waweze kujikimu kimaisha.
Akizungumza na Zenj fm Radio baada ya Mahafali hayo Mkuu wa Chuo
hicho Kamoto Abdul Hassan amesema wataendeleza juhudi zao katika kutoa
elimu inayoendana na mahitaji katika soko la ajira ili wanafunzi
wanaomaliza waweze kunufaika na elimu wanazopewa vyuoni mwao.
Aidha amesema kutokana na Wananfunzi wa Zanzibar wamekuwa na mwamko
mkubwa wa kujifunza fani mbalimbali ni vyema kwa vyuo binafsi kueka
ushindani katika kuwapatia wananfunzi elimu bora na inayotambulika
wakati wa kutafuta ajira.
Nao wananfunzi waliomaliza masomo yao chuoni hapo wamesema
watahakikisha wanatumia vyema mafunzo wanayoyapata katika kutafuta njia
za kujiari na kutowa wito kwa wananfunzi wenzao kuachana na tabia ya
kusubiri ajira kutoka serikali jambo ambalo linarejesha nyuma shughuli
zao za maendeleo.
Jumla ya wahitimu 157 wamemaliza masomo yao katika chuo hicho
wakiwemo wanafunzi Ngazi ya Cheti na Stashahada kwa fani ya Teknolojia
ya Habari na Mawasiliano na Ununuzi na Ugavi.
chanzo:Zanzibar24.
Comments