
Akizungumza na Zanzibar24 Mkurugenzi wa Jumuiya ya Wanasheria
wanawake Zanzibar Zafela Jamila Mahmoud amesema hali hiyo
inarejesha nyuma kwa wanawake kufikia malengo yao kwani sheria
nyingi zilizopo sasa ambazo hazijatia mkazo mali za wanawake hasa
wakati wa ndoa zinapovunjika.
Amesema kesi nyingi zinazopokelewa katika Jumuiya hiyo zinatokana
na wanawake wengi kutokuwa na hati maalum ya umiliki wa mali pamoja
na kuwepo tabia ya kuaminiana bila ya maandishi kwa wanandoa.
Hivyo amesema ili kukabiliana na tatizo hilo Serikali na Asasi za
kiraia hazinabudi kutoa elimu maskulini na katika jamii juu ya
umuhimu wa kuwepo kwa mikataba ya umiliki wa mali kwa wanandoa.
Jumla ya kesi sita zilipokelewa katika Jumuiya hiyo kuanzia mwaka
jana hadi septemba mwaka huu ambapo kesi tano zilifikishwa mahakaman na
kesi moja imepatiwa usuluhishi.
chanzo:Zanzibar24
Comments