Wizara ya Elimu Zanzibar kuajiri walimu wa maandalizi.



Wizara  ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imesema itaendelea kuajiri walimu wa maandalizi ili kuweza kuleta ufanisi mkubwa kwa wanafunzi.

Akizungumza na wahitimu wa ngazi ya uwalimu wa maandalizi katika mahfali ya pili ya mradi wa ‘' watoto kwanza '' huko katika ukumbi wa sameil academy gombani chake chake Pemba Naibu Warizi wa elimu na mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Mmanga Mjengo Mjawiri amesema Serekali imekabiliwa na changamoto ya ukosefu wa walimu wa maandalizi hivyo kupitia wahitimu hao wataweza kutoa ajira ili kuleta mabadiliko makubwa katika maeneo yao.


Amesema upungufu wa walimu wa maandalizi upo na sasa kuna pengo kubwa amabalo linafikia zaidi ya 536 kupitia wahitimu hao wataweza kutoa ajira ili kuziba pengo ambalo linaonekana kudhofisha wanafunzi wa maandalizi hapa Zanzibar.

Amesema ili mwalimu awezekuleta mabadiliko nivyema abadilike kwakutoa elimu inayo endana na wakati nakuweza kutanua wingo mpana kwa wananfunzi.

Aidha amewaomba wahitimu hao kuyatumikia vizuri mafunzo walioyapata ili iwe matunda bora kwa wanafunzi wa maandalizi wamaokwenda kuwatumikia.

Kwaupande wake mkurugenzi wa Madrasa Early Childhood Programme Zanzibar Nd.Khamis Abulla Said  amesema licha ya kuwepo changamoto mbali mbali zinazo wakabili katika kutoa taaluma kwa walimu lakini bado wanaendelea kupambana nanzo.

Amefahamisha kuwa kwa kushirikiana na shirika la UNICEF  agakan fodation na  Dubai care wameweza kufadhili mafunzo mbali mbali ambayo yamewasaidia kutoa elimu kwa walimu wa maandalizi wapatao 970.

Awal akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wenzake Zuhra Suleiman Issa amesema changamoto kubwa wanayo kabiliananayo ni ukosefu wa ajira jambo ambalo linawarudisha nyuma na kukatisha tamaa katika fani yao.

Jumla ya wahitimu wapatao 373 katika gazi ya uwalimu wa maandalizi wamekabidhiwa vyeti kati ya hao 117 ni wale waliomaliza miaka miwili na 256 wamemalizamasomo yao ya miezi sita kupitia mafunzo kazini.
 

Comments