Wazazi watolewa wasi wasi juu ya fedha wanazo tozwa watoto maskulini.

Related imageMkuu wa Wilaya ya Kaskazini  B Issa Juma Ali amesema  kutoleshwa michango kwa wanafunzi wa skuli ya Bumbwini makoba haihusiani na michango iliyoondoshwa na serikali.
Akizungumza na Zanzibar24 kufuatia  wazazi kulalamika  kutozwa michango katika skuli hiyo amesema kuwa michango inayotozwa kwa wanafunzi ni kutokana na kuwepo kwa upungufu wa vyoo katika skuli hiyo.

Amesema kuwa kuna baadhi ya wananchi  hawana utamaduni wa kutoa  michango  midogo midogo  katika  skuli hali ambayo  inazorotesha  maendeleo  ya skuli hiyo.
Aidha Mkuu huyo amefahamisha kuwa Wilya hiyo imeandaa mpango wa kutoa elimu kwa wazazi na walezi juu  ya kutoa  michango ambayo itasaidia  katika skuli mbalimbali ili  kukabiliana na matatizo yanayojitokeza.
chanzo:Zanzibar24

Comments