
Wawili hao ambao hawajatajwa na serikali
wanatoka katika kijiji kimoja maskini Kusini mwa Guangxi na walikuwa
wakijaribu kwenda kwa wazazi wao wanaofanya kazi katika mkoa jirani wa
Guangdong.
Waliripotiwa kwamba wametoweka mnamo tarehe 23 Novemba
na mwalimu wao na kupatikana siku hiyohiyo chini ya gari hilo katika
kituo kimoja cha mabasi.
Picha na kanda za video zinaonyesha vijana hao waliojaa matope na wakining'inia chini ya basi hilo.
Kulingana
na gazeti la Southern Morning (Nanguo Zaobao), wavulana hao wana umri
wa kati ya miaka minane na tisa na walipatikana na maafisa wa usalama
wakati basi hilo liliposimama katika kituo kimoja.
Walikuwa tayari wamesafiri katika maeneo yenye milima kwa takriban maili tatu huku wafanyikazi hao wakibaini kwamba hawakuumia.
Miili
ya watoto hao ilikuwa myembamba mno hivyobasi eneo la chini la basi
hilo lilikuwa eneo zuri la kujificha , mfanyikazi mmoja aliliambia
gazeti hilo.
Wafanyikazi wanasema kuwa wavulana hao walikataa kuzungumza walipohojiwa.
Lakini
mfanyikazi mmoja aliliambia gazeti la Southern Morning: Baadaye
tulielewa kwamba wavulana hao walikuwa wakitaka kuonana na wazazi wao.
Walijificha chini ya basi hilo kwa sababu walitaka kuwaona wazazi wao.
Ripoti zinasema kuwa watu wa jamii yao waliarifiwa na vijana hao wakachukuliwa siku hiyohiyo.
chanzo:BBc.
Comments