Watendaji wa Serikali wahimizwa kufanya kazi kwa ufanisi.

Katibu mkuu ofisi ya makamo wa pili wa Rais Dkt Idrissa Muslim Hijja amewataka maofisa na wafanyakazi  katika taasisi mbali mbali za serikali mkoa wa kusini unguja kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu za utumishi serikalini.

Dkt Idrissa ametoa kauli hiyo katika nyakati tofauti ikiwemo makunduchi, kitogani na dunga ikiwa ni muendelezo wa  ziara za  kuwaaga maofisa, wafanyakazi na watendaji wa halmashauri  za wilaya  zilizomo ndani ya mkoa huo.

Amesema kufanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni kwa wafanyakazi na watendaji wa serikali ndio njia pekee itakayoweza kuleta ufanisi na mafanikio makubwa kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
Aidha dkt Idrissa amewataka watendaji hao hasa wakurugenzi wa halmashauri kusimamia vyema utekelezaji wa mpango wa serikali wa kukasimu madaraka kutoka serikali kuu kwenda serikali za mitaa ili kutimiza vyema azma ya serikali katika kurahisisha upelekaji wa huduma za kijamii kwa wananchi.
Nae kaimu mkuu wa mkoa huo mhe, Idrissa kitwana mustafa amemshukuru katibu huyo kwa mashirikiano mazuri aliyotoa kwa viongozi na watendaji katika kipindi chake chote cha uongozi wake ambapo ameahidi kuyaendeleza na kusimamia vyema utekelezaji wa majukumu ya serikali hususan katika suala zima la migogoro ya ardhi.
chanzo:zanzibar24.

Comments