Hatua hiyo imekuja kukiwa kumesalia siku tatu pekee uchaguzi huo mdogo kufanyika, huku chama hicho kinachowania kukitetea kiti hicho kikikabiliwa na ushinda kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kilichomsimamisha, Godfrey Misana.
Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu leo Novemba 22, Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Raymond Mwangwala amewataja viongozi wengine wa Kitaifa wanaotarajiwa kuwasili mwanza kuanzia leo kuwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi, Abdallah Bulembo na mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde “Kibajaji”
Amesema pamoja na kusaidia kampeni na mikakati kuhakikisha mgombea wa chama hicho, Constantine Sima ananyakua kiti hicho viongozi hao pia wanatakwenda kufanya kampeni katika Kata ya Kiijima Wilayani Misungwi ambako pia kuna uchaguzi.
Kiti cha udiwani Kata ya Mhandu kilibaki wazi tangu Aprili 7, kutokana na kifo cha aliyekuwa diwani kupitia CCM. Lucas Wambura.
“Ni dhamira ya CCM kukitetea kiti cha udiwani Mhandu; tuna wanachama zaidi ya 11, 000 ambao ni sawa na asilimia 79 ya wapiga kura zaidi ya 14, 000 wanaotarajiwa kushiriki uchaguzi wa Jumapili Novemba 26. Hii inatuhakikishia ushindi wa kishindo,” ametamba Mwangawala
Wakati CCM ikiongeza nguvu dakika za lala salama, vyama vya Chadema na ACT-Wazalendo tayari imewatumia viongozi wao wa Kitaifa kuwanadi wagombea wao katika kata hiyo.
Novemba 17, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema na Katibu Mkuu wake, Dk Vincent Mashinji pamoja na viongozi wengine wa kitaifa na Kikanda walikuwa Mhandu kumnadi mgombea wa chama hicho, Godrey Misana.
Vivyo hivyo, Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, naye tayari amefika Kata ya Mhandu kumnadi mgombea wa chana hicho, Emily Balahula.
Hata hivyo, mchuano mkali unashuhudiwa kati ya wagombea kutoka vyama vya CCM na Chadema ambao wanaendesha kampeni za kila siku majukwaani na nyumba kwa nyumba kushawishi wapiga kura huku ajenda kuu kwa vyama vyote ikiwa ni maendeleo katika sekta za afya, maji na miundombinu ya barabara.
chanzo:mwananchi.
Comments