
Wito huo ameutoa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya
uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha miaka miwili ndani ya Jimbo la Kikwajuni
Unguja.
Amesema vijana wanatakiwa kuwa wabunifu katika kukabiliana na
changamoto ya ukosefu wa ajira kwa kujiunga na vikundi mbali mbali
vinavyoanzishwa katika jimbo hilo ili kujikwamua kimaisha.
Amesisitiza umuhimu wa vijana wa UVCCM kujiendeleza kielimu katika
fani mbali mbali kwani kufanya hivyo kutasaidia jumuiya kuwa na vijana
imara wenye ujuzi utakaosaidia kuharakisha maendeleo ya umoja huo kwa
haraka.
Pia amewashauri vijana hao kuwa kuwa wamoja na wenye msimamo
usioyumba katika kupigania maslahi ya CCM ili iweze kushinda katika
Uchaguzi Mkuu ujao.
“CCM ndio chama pekee kinachojali na kuwalea vijana katika misingi
imara ya kuwajenga kifikra, kiitikadi na kimaadili ili waweze kuwa
viongozi bora wa baadae watakaoendeleza urithi wa Wanamapinduzi ya Mwaka
1964 kwa vitendo.”, alisema Mwenyekiti huo.
Akizungumzia tatizo la matumizi ya Dawa za kulevya, Mwenyekiti huyo
wa UVCCM alisema Wilaya ya Mjini imekuwa ni miongoni mwa sehemu
zilizoathirika na janga hilo hivyo vijana wanatakiwa kujiepusha na
matumizi ya dawa hizo kwani zinaangamiza nguvu kazi ya taifa.
Naye Katibu wa Wilaya hiyo Aboud Said Mpate , alisema lengo la ziara
hiyo ni uongozi huo kutoa shukrani kwa wanachama waliowachagua viongozi
hao pamoja na kupokea taarifa za utekelezaji wa Ilani kutoka kwa
Wabunge, Wawakilishi na Madiwani wa Wilaya ya mjini ili wananchi
waliowachagua waweze kujua mambo yaliyotekelezwa kwa kipindi cha miaka
miwili.
Aboud amewataka vijana hao kuwa makini kwa kuepuka kutumiwa katika
kutengeneza makundi ya kulinda maslahi ya baadhi ya viongozi hasa wakati
huu wa uchaguzi unaoendelea ndani ya Chama na Jumuiya zake.
Akizungumzia utekelezaji wa Ilani, Mwakilishi wa Jimbo hilo, Nassor
Salim Jazeera amesema viongozi wa jimbo hilo kwa kushirikiana
wameanzisha miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo kuendeleza mradi wa
maji wenye thamani ya zaidi ya milioni 300, kuanzisha vikundi vya usafi
ili vijana wasiokuwa na ajira wajiajiri wenyewe.
Mh. Jazeera alisema miradi mingine wameshauri na kushirikiana na
serikali kujenga barabara za lami mbili, ujenzi wa uwanja wa michezo
wa Mao Tse Tung, Ujenzi wa Shule ya kisasa ya Ghorofa katika Mtaa wa
Mwembe shauri pamoja na kuwasaidia akina Mama mitaji ya kuanzisha
vikundi vya ujasiriamali.
Alifafanua kuwa lengo la viongozi hao ni kuhakikisha wanamaliza kero
na changamoto zote zinazowakabili wananchi katika jimbo hilo kabla ya
mwaka 2020.
Sambamba na hayo alisifu kasi ya kiutendaji ya UVCCM katika Wilaya
hiyo na kuwasihi waendelee kushirikiana na viongozi hao bega kwa bega
ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali chini ya Uongozi wa
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein.
Ziara hiyo ya siku nne itaendelea kufanyika katika Majimbo yote ya UVCCM Wilaya ya Mjini Zanzibar.
![]() |
Comments