Tatizo la maji lazorotesha shughuli za wananchi Mtendeni.

Mamlaka  ya Maji Zanzibar  ZAWA imeombwa  kuwatatulia tatizo la ukosefu wa maji linalowakabili waakazi wa kijiji cha Mtende lililodumu  kwa  muda mrefu katika kijiji chao.

Wakizungumza  na Zanzibar24 wananchi hao  wamesema   tatizo hilo   limekuwa  likiwaathiri   kwa kiasi  kikubwa    kwani  hutumia   muda mrefu   wa kutafuta  huduma hiyo  katika  vijiji jirani   badala  ya kuendelea na  shughuli  za  kujitafutia maendeleo.

Wamefahamisha kuwa   kisima chao  cha kusambazia maji  kilichopo  hivi sasa ni cha muda mrefu  na  miundombinu yake   imeshachakaa ambayo ipo tokea  miaka 60  na kubwa zaidi  kimeshazidiwa na idadi ya  watu wanaoishi katika kijiji hicho na kupelekea huduma hiyo pia kukosekena  hadi walindie.
Nae  Sheha wa Shehia hiyo Khamis Ramadhani Mbaraka amekiri kuwepo kwa tatizo   la maji  kwa zaidi ya miezi sita  na kuyataja maeneo ambayo  huduma  hiyo kwa sasa hawaipati  kabisa  ikiwemo maeneo ya pemba,cheju na ndani ya mtende.
Hivyo  Sheha  huyo ametoa wito kwa  Mamlaka  husika  kulifanyia  ufumbuzi  tatizo hilo kwa haraka kwani  shughuli za wananchi  nyingi zimekuwa zinakwama kutokana na muda mwingi huutupa kwa ajili ya kutafuta maji kwa mahitaji ya  nyumbani.
chanzo: zanzibar24

Comments