Na Lilian Lundo, Dodoma
Serikali
kupitia Halmashauri za Wilaya katika mwaka 2016 imetoa jumla ya Hekta
271,882.86 za ardhi kwa vijana nchi nzima ili kufanya shughuli za
uzalishaji mali na kujipatia ajira.
Hayo
yameelezwa jana, Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera, Bunge, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Anthony Mavunde alipokuwa
akijibu swali la Mbunge Viti Maalum Mhe. Aida Khenan juu ya mpango wa
Serikali kwa vijana wanaomaliza shule za msingi, Sekondarii na Vyuo kwa
kuwazesha kujiajiri.
“Serikali
imeendelea kuimarisha utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ambao
unalenga kuwasaidia vijana wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu kuweza
kujiajiri kwa kuwapa mikopo ya masharti nafuu na mafunzo ya
ujasiriamali,” alisema Mavunde.
Aliendelea
kwa kusema, katika kipindi cha mwaka 2013/2014 hadi 2016/17, Serikali
kupitia mfuko wa Maendeleo ya vijana imetoa mikopo ya masharti nafuu ya
Shilingi Bilioni 5.8 kwa vikundi vya vijana 6,076 vyenye wanachama
30,380 katika Halmashauri za Wilaya 157 kupitia SACCOS za Vijana.
Aidha
Mavunde alisema, kupitia programu ya kukuza ujuzi wa nchi Serikali
imeanzisha utaratibu maalum wa kutambua ujuzi uliopatikana kupitia mfumo
usio rasmi na kuurasimisha kwa kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa wale
walio tayari kuhitaji na kuwapa vyeti vinavyotambulika.
“Utaratibu
huu unawapafursa vijana wetu ya kuendelea na mfumo rasmi wa mafunzo na
pia kutambulika na waajiri au watoa kazi,” alifafanua Mavunde.
Vilevile
alisema, Serikali imerahisisha utaratibu wa uundaji wa Makampuni
kupitia BRELA hivyo vijana wengi wanaomaliza vyuo kuweza kuanzisha
Makampuni na biashara zinazowezesha kuajiri vijana wengi.
Hata
hivyo, Mavunde amewataka vijana wanaomaliza shule za msingi na
sekondari kujiunga katika vikundi vya kuzalisha mali na kusajiliwa rasmi
kupitia sheria ya usajili wa NGOs.
Aidha mpaka sasa jumla ya vikundi vya vijana vya uzalishaji mali 10, 200 vimesajiliwa.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments