Waziri
wa Madini, Angela Kairuki amesema kuwa serikali inataraji kupata
mrabaha zaidi katika madini ya Almasi yaliyokamatwa katika uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere kutoka kwa Kampuni ya Williamson
Diamond iliyokuwa ikitaka kutoroshwa madini nchini kwenda Ubelgiji.
Waziri
Kairuki amesema hayo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari
wakati akitoa ripoti ya Wizara ya Madini juu ya mzigo huo wa Almasi
kutoka kampuni ya Williamson Diamonds.
“Tarehe
20/10/2017 almasi hizo zilisafirishwa kwenda ubelgiji na serikali
ilituma maafisa wake kusimamia uuzwaji wa alamasi hizo ambapo tarehe
7/11/2017 almasi hizo ziliuzwa kwa dola za Marekani 10,261,227.76 hivyo
thamani hii ni ongezeko la Dola za Marekani 2,069,582.77 sawa na
asilimia 20.16%”amesema.
Amesema
kutokana na ongezeko hilo baada ya almas kuuzwa serikali itapata
mrabaha zaidi ambao ni mwisho kiasi cha Dola za Marekani 124,174,.97 na
ada ya ukaguzi Dola za marekani 20,695.83 ambayo jumla yake ni dola za
Marekani 144,870.80 sawa na shilingi Milioni 325.525 hivyo jumla ya
mapato yote ya serikali kutokana na mauzo ya almasi hizi ni Dola za
Marekani 718,288.95
Aidha
Waziri Kairuki amesema katika mzigo huo waliweza kuikuta Almasi moja
yenye rangi ya pinki ambayo ni adimu kupatikana na yenye uzito wa
karatani 5.92 na kuuzwa kwa dola za marekani 2,005,555.00 sawa na
shilingi Bilioni 4.51 .
Alimaliza
kwa kusema kuwa anawakikishia Watanzania kuwa serikali itaendelea
kuisimamia kwa makini rasilimali zetu za madini ili kuhakikisha kuwa
nchi yetu inanufaika ipasavyo.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments