Akizungumza na Zanzibar24 Mratibu wa Kampeni ya kuhamasisha wanawake
na kutoa elimu ya kutengeneza bidhaa mbalimbali za ujasiriamali Abla
Mohammed Baraka amesema kwa kiasi kikubwa wanawake wamekuwa
wakichangia pato la taifa hivyo ni vyema kusimama imara katika
kujiunga na vikundi vya ushirika ili waweze kujikimu na kuondokana na
utegemezi.
Amesema utegemezi wa wanawake katika familia unachangia kwa kiasi
kikubwa kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji hivyo nivyema kujiamini
katika kufanya shughuli za maendeleo ili kuweza kujikwamua na hali
ngumu ya maisha.
Aidha Abla ameiyomba Serikali kuendelea na juhudi zake za kutoa
fursa kwa wanawake za kuwapatia mitaji hasa katika vikundi vya
ushirika ili waweze kujiendeleza katika kazi zao kwani baadhi yao
hushindwa kutokana na kutokuwa na mitaji.
Kampeni ya kuhamasisha wanawake ijulikanayo kwa jina la wanawake
chakarika imekuwa ikitoa elimu mbalimbali kwa wajasiriamali ili
waweze kupata ujuzi zaidi ikiwemo utengenezaji wa Sabuni za aina
tofauti na utafutaji wa masoko.
chanzo:Zanzibar24
Comments