
“Nimeisubiri kwa shauku kubwa siku hii ya leo ili nipate fursa ya
kupigania mageuzi ya kisiasa na ya kiuchumi Tanzania,” amesema Nyalandu
baada ya kukabidhiwa kadi.
Amesema ana shauku, furaha na heshima kukaribishwa rasmi kuwa
mwanachama wa Chadema. Nyalandu ameongeza kuwa katika majira na nyakati
ambazo Taifa linapitia, mabadiliko ya kisiasa nchini Tanzania ni lazima.
“Naungana na chama hiki pendwa ili tutembee pamoja mtaa kwa mtaa
kijiji kwa kijiji tuwaambie wananchi wakati wa ukombozi ni sasa,”
alisema Nyalandu.
chanzo: zanzibar24.
Comments