
Ushauri huo aliutoa wakati akizungumza na wananchi wa shehia za
Tumbatu, katika ziara yake ya kuyatembelea maeneo mbalimbali ya mkoa huo
yenye lengo la kusikiliza kero za wananchi.
Alisema muda mrefu wakaazi wa kisiwa hicho wamekuwa wakitofautiana na
kusababisha maendeleo kudumaa, hivyo kuna haja ya kuweka pembeni
tofauti hizo na kufanya kazi pamoja kwa umoja wao.
Alisema masuala ya siasa, yamewafanya wakaazi wa kisiwa hicho
kusambaratika, lakini akawambia kuwa siasa ni mambo yanayokuja na
kupita, lakini umoja na mshikamano utabakia daima hasa ikizingatiwa wote
ni ndugu wa mama na baba mmoja.
Aidha alisema historia ya kisiwa hicho inaonesha wakaazi wake ni
wamoja, hivyo kuna haja umoja huo kuendelezwa na wasikubali kugawanywa
kwa sababu ya tofauti za kisiasa.
“Tumetenganishwa wakati tushajitawala, wazee wangu nawaomba
tusikubali kusambaratishwa, kwa sababu yoyote ile, sisi ni wamoja na
daima tutaendelea kuwa wamoja, tujitathmini tulipokosea ili
turekebishe,” alisema.
Aliwahimiza kuendelea kushirikiana kwenye shughuli za maendeleo na kijamii, kama harusi na maziko na kuacha kubaguana.
Alisema changamoto zinazokikabili kisiwa hicho zitaondoka, kama
wananchi watashirikiana na kamwe wasitarajie kwamba mtu kutoka nje
anaweza kuja kutatua changamoto zao.
Nae Zubeir Bakari Ali mwananchi wa shehia ya Jongowe, alisema
wamefarajika kumuona Mkuu wa Mkoa kufika katika kisiwa hicho kusikiliza
matatizo yanayowakabili.
“Hakika tunaandika tarehe muhimu sana na hii haifutiki maana hatujawahi kumuona kiongozi wa ngazi kama yako,” alisema.
chanzo:zanzibar24.
Comments