
Kwamujibu wa taarifa zilizopatikana kwa waliokuepo karibu na tukio
hilo na kuthibitishwa na kaimu Kamanda wa Polisi ambae pia ni Mkuu wa
upelelezi mkoa wa Kaskazini Unguja Suleiman Hassan amesema tukio hilo
limetokea saa sita na nusu Mchana hapo jana wakati marehemu huyo alikuwa
anashuhulika katiaka harakati zake za kuogelea.
Amefahamisha kuwa kabla ya kifo chake marehemu alifika katika Hoteli
ya Paradise huko Nugwi akiwa katika shuhuli za kuogelea ndipo
alipozidiwa na maji nakufariki dunia hapo hapo.
Kaimu Kamanda ameendelea kutoa wito kwa wamiliki wa hoteli waweke
watu karibu na maeneo hayo ambapo likitokezea tatizo kama hilo iwe
nirahisi kuwahi mapema kabla tatizokubwa kutokezea.
chanzo: zanzibar24.
Comments