Jeshi
la Polisi limefanya upekuzi Makao Makuu ya Chama cha ACT- Wazalendo na
kuchukua nyaraka, vifaa vya kiilektonikia vilivyotumika kuandaa taarifa
ya kusinyaa kwa uchumi wa nchi.
Mbali
na kufanya upekuzi, Jeshi hilo linaishikilia simu ya mkononi ya
Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe kwa upelelezi huku yeye akisema
mawasiliano aliyokuwa akiyafanya yamezingatia uhuru uliopo katika
Katiba.
Upekuzi
huo ulifanyika jana mchana muda mfupi baada ya Zitto kwenda kuripoti
Kitengo cha Uhalifu wa Makosa ya Kifedha-Kamata jijini humo na kutakiwa
kurejea tena Novemba 21.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu amesema ‘’polisi
walifika hapa saa 6 na wamefanya upekuzi na wamechukua flash, laptop
(kompyuta mpakato) na nyaraka ambazo ni taarifa kwa umma iliyotolewa
kuwa tutakutana kujadili hali ya uchumi.”
Ado
amesema upekuzi huo ulitumia muda mrefu baada ya polisi hao aliodai
walikuwa wanne kufika na Katibu Mkuu wa chama hicho, Doroth Semu
kutomkuta hivyo wakaamua kumfuata nyumbani kwake Tabata.
“Walisema
watakwenda kufanyia kazi vifaa hivyo na watavirejesha haraka ila
hawajasema hasa ni lini...wale polisi mmoja alivaa sare na watatu
walivaa kiraia ,” ameongeza
chanzo:Mpekuziblog.
Comments