Aliyekuwa
mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu leo ataungana na viongozi
wa Chadema kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani utakaofanyika
katika kata 43 nchi.
Akizungumza
jana Novemba 11, kwenye ufunguzi wa kampeni hizo Kimara Suka jijini Dar
es Salaam, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe alisema amempokea
Nyalandu na ataungana naye kwenye mkutano mwingine kama huo
utakaofanyika Mtwara mjini leo.
‘’Kila
anayeondoka chama tawala anaitwa fisadi, potelea mbali wamempokea na
wengine wengi watahamia kuleta mabadiliko’’ alisema na kuongeza
"Mabadiliko
hayaji ghafla yanakuja taratibu na ujio wao ndiyo mwanzo wa
mabadiliko tulipoanza na tulipo sasa kuna tofauti kubwa" amesema
Mbowe.
Alifafanua
kwamba haungi mkono nchi kuwa na wezi, lakini anashauri sheria iachwe
iamue haki badala ya kuingiliwa kama inavyofanyika kwa mahakama.Huku
akidai kwamba watawala wana hofu ndiyo maana hawataki ushauri.
Alisema
wataendelea kupigania haki ya kupigania haki ya kufanya mikutano ya
kisiasa na ipo siku wataingia mtaani kuidai bila kuogopa vifaru.
Alisema huu siyo wakati wa kuogopa na kukaa kimya ni wakati wa kusimama na kutetea haki ya kufanya siasa.
Kuhusu
uchumi kusinyaa alisema ni kweli umesinyaa na inaonekana wazi jinsi
maisha yalivyo wananchi, wafanyabiashara, watawala wote wanalia njaa
hakuna mwenye nafuu.
Meya
wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob alisema anahitaji kuongeza nguvu
ya kuleta maendeleo katika manispaa hiyo, hivyo mgombea udiwani kata
ya Saranga Ephram Kinyafu anatosha.
Naye Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani Frederick Sumaye alihoji kuhusu hali za wananchi kuendelea kuwa mbaya.
"Tumeamua na tunamaanisha wakati huu ushindi ni lazima, na mtakaotupa ushindi ni nyie wananchi" alisema Sumaye.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments