Mbunge
wa Mtama, Nape Nnauye, amekiri kuwepo na vitendo ambavyo siyo sahihi
ambavyo vilivyojitokeza katika Uchaguzi wa marudio katika baadhi ya
kata na kutaka hatua za kisheria zichukuliwe.
Nape
amefafanua hayo baada ya kuwepo na malalamiko hayo kutoka upande wa
upinzani ambapo amesema kwamba vitendo hivyo vinapaswa kushughulikiwa
kisheria kama wahalifu na siyo kushughulikiwa kisiasa na kwamba kufanya
matendo hayo kisiasa ni njia za kuficha uovu.
Pamoja
na hayo Nape ameongeza kwamba hajawahi kuwa muumini wa matumizi ya
nguvu kwenye siasa na wala hajawahi kushiriki mipango ya kutumia nguvu
bali anaamini katika matumizi zaidi ya nguvu.
Aidha
Nape ameongeza kwamba sehemu zote alizofanya kampeni na wala hakubariki
matumizi ya nguvu hivyo kuwashauri vyama vya upinzani wafanye tathmini
ya kweli kisha kuchukua hatua pale walipoteleza katika uchaguzi.
"Rafiki
zangu Upinzani fanyeni tathmini ya kweli halafu chukueni hatua pale
mlipoteleza. Hichi kinachoendelea cha kutoa visingizio vya jumla.
Sikatai kuwa kulikuwa na baadhi ya maeneo kumekuwa na vitendo si vya
kibinadamu lakini si kwa kata zote. Vitendo hivyo vishughulikiwe
specific kisheria kama wahalifu na si kushughulikiwa kisiasa".Amesema
Nape
chanzo:Mpekuziblog.
Comments