Mwalimu wa kike mwenye miaka 40 katika shule ya Sekondari ya St. Charles
High School mjini Maryland nchini Marekani amehukumiwa kifungo cha
mwaka mmoja jela kwa kosa la kumtongoza na kumtumia picha za utupu
mwanafunzi wake wa kiume mwenye umri wa miaka 17.
Kwa mujibu wa maelezo kutoka kwenye mtandao wa kituo cha runinga cha Fox 5 DCMwalimu
huyo aliyetambulika kwa jina la LaToya Nicole Parker (40) imeelezwa
kuwa alikuwa anamtuma mwanafunzi huyo kwenye supermarket kipindi cha
mapumziko na kwenda nae nyumbani kwake.
Kisa hicho ambacho kiliripotiwa na wazazi wa mwanafunzi huyo mwezi
machi mwaka huu, 2017 kwenye kituo cha polisi kabla ya kupelekwa
mahakamani ambapo mshtakiwa alikiri kutenda kosa hilo jumatatu ya wiki
iliyopita.
Upelelezi uliofanywa na polisi pamoja na ushahidi uliotolewa
mahakamani unaonesha kuwa mwalimu huyo alianza kumtongoza mwanafunzi
huyo tangu mwezi April mwaka huu , 2017 kwa kumuandikia barua za mahaba,
kumtumia picha zake za utupu na kumuahidi pesa mwanafunzi huyo kama
angelikubali.
Kwa upande mwingine mwalimu mkuu wa shule ya St. Charles High School
Principal, Richard Conley amesema mwalimu huyo alikuwa anafundisha somo
la Mapishi shuleni hapo na alikuwa hajaajiriwa rasmi shuleni hapo bali
alikuwa anafanya kazi kwa muda (Temporary) tangu mwezi Machi mwaka huu
2017.
“Baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wazazi wake mapema
tulimsimamisha kazi Ms. Parker kwani tayari walikuwa wameshatoa taarifa
polisi ili kupisha uchunguzi.“amesema Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Richard Conley.
Polisi mjini Maryland wamesema walikuta picha 5o za utupu za mwalimu
huyo na jumbe 303 zilizotumwa kwenye simu ya mwanafunzi huyo nyingi
zikiwa za mahaba.
Mahakama mjini Maryland inayoshughulikia kesi za watoto imetoa hukumu
kwa mwalimu huyo kwenda jela mwaka mmoja au kulipa faini ya dola
$20,000 sawa na Tsh milioni 44 kwa kosa la kusambaza picha za utupu kwa
watoto na udhalilishaji.
Vyanzo : Fox 5 DC & The Bay Net na zanzibar24.
Comments