
Akizungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na Mkutano huo Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari ZPC
Abdallah Abdlrahman mfaume amesema kutokana na vyombo vya habari kuwa
na uwezo mkubwa wa kuimarisha ukuwaji wa Uchumi Nchini ni vyema
kuendelea kushirikishwa katika utoaji wa taarifa muhimu.
Amesema kutokana na Serikali ya Zanzibar
kuwa katika harakati za kufikia uchumi wa kati Mkutano huo pia utawapa
fursa waandishi wa habari kujifunza dhana ya uchumi wa viwanda na uchumi
wa kati katika kuandika habari zitakaimarisha maendeleo Nchini.
Aidha amesema mkutano huo pia utaifanyia
marekebisho katiba ya mwaka 2003 ili iweze kuendana na matakwa na
mahitaji wa wananachama katika kuendeleza ufanisi wa kufanya kazi katika
jamii.
Hata hivyo ametowa wito kwa waandishi wa
habari kuendeleza mashirikiano katika utendaji wa kazi zao pamoja na
kujiunga na chama hicho ili kunufaika na fursa zilizopo ikiwemo
kushiriki mafunzo ya kuengeza ufanisi katika utendaji wa kazi zao.
Kwa upande wake Kaimu katibu mkuu wa Chama
hicho Mwinyi Mvua Abdi Nzukwi amesema licha ya mafanikio yaliopatikana
chama hicho lakini kumekuwa na tatizo la ushiriki mdogo wa Waandishi wa
habari katika kuendeleza chama hicho.
Amesema ili kufikia malengo yaliyokusudiwa
ni vyema kwa waandishi wa habari kuwa mstari wa mbele katika
kukiendeleza chama hicho pamoja na kuendelea kuandika habari zenye
ukweli katika kuendeleza amani iliopo.
Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na
viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa ambapo waziri wa fedha na
Mipango anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmin katika mkutano huo wenye ujumbe
usemao Vyombo vya Habari ni Chachu ya kufikia Uchumi wa Viwanda Vishirikishwee.
chanzo:zanzibar24.
Comments