
Akizungumza mbele ya Mahakama hiyo Mwanasheria wa kujitegemea Ahmed
Mohammed amesema kasi ya kuongezeka kwa maovu yakiwemo
uhalifu,ukahaba,udhalilishaji unachangiwa na uwepo wa mabaa nchini
yasiyokuwa na sifa ya kufanya biashara hiyo.
Amefahamisha kuwa licha ya kuwa serikali inategemea pato lake
kupitia biashara ya pombe lakini iwatizame wananchi kwa jicho la
huruma kwani wamekuwa waathirika wakubwa wa mabaa hayo yaliyopo
karibu na makaazi ya jamii.
Amesema endapo serikali itapunguza utoaji wa ruhusa za biashara
hiyo itasaidia kupunguza utitiri wa mabaa nchini hasa katika maeneo
ya makaadhi ya watu na kulinda maadili ambayo yanaonekana kupotea kwa
kasi kubwa.
Zaidi ya wananchi mia tatu walijitokeza kuweka pingamizi zao katika Mahakama ya Vileo ya Wilaya ya Makunduchi Mkoa wa kusini.
chanzo:Zanzibar24
Comments