Madudu yafanyika vyumba vya mitihani Zanzibar.

Mwanamke mmoja alijulikanwa kwa jina la Grace Steven Maganga (20) mkaazi wa Jang’ombe alikamatwa katika chumba cha mtihani cha  Sun City kilichopo Mji Mkongwe.

Tukio hilo lilitokea juzi asubuhi majira ya saa 3:30 Mjimkongwe wilaya ya mji.


Akithibitisha kutikea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Maghari, Hassan Nassir Ali, alisema kijana huyo alitiwa mikononi akiwa katika harakati za kumfanyia mtihani, Rukia Bukuku Laurence ambae ni mjamzito.

Alisema baada ya uchunguzi kukamilika mtuhumiwa huyo atafikishwa katika vyombo vya sheria kujibu tuhuma zinazomkabili.

Ofisa Elimu mkoa huo, Khatib Tabia Muhsin, akizungumzia kadhia hiyo alisema suala la udanganyifu wa mtihani lina athari kubwa kwa skuli na mwanafunzi hivyo akawataka kujiepusha.

Kuhusu madai ya kuwepo wanafunzi sita katika skuli ya Mpendae kuzuiliwa kufanya mtihani wa kemia, alisema madai hayo si ya kweli na wanafunzi wanaendelea kufanya mitihani yao kama kawaida.

Kuhusu wanafunzi wanoshindwa kufanya mitihani kwa sababu ya kuumwa, alisema taratibu zimewekiwa ikiwemo mzazi kwenda kwa daktari aliyemtibu mwanafunzi huyo na kumuandikia barua kuhusu ugonjwa wake ili hatua zichukuliwe.

Chanzo: ZanzibarLeo na zanzibar24.

Comments