Mbunge
wa Arusha Mjini, Godbless Lema amemshauri Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Job Ndugai kutumia busara kuwaondoa bungeni
wabunge nane walioingia bungeni kuziba nafasi za wabunge nane waliokuwa
wamevuliwa uanachama wa chama cha CUF Julai 24.
Lema
ametumia mtandao wake wa kijamii kuandika ujumbe huo ikiwa ni siku moja
baada ya Mahakama Kuu kutengua uamuzi wa kufukuzwa kwa Wabunge 8 na
Madiwani 2 wa Chama cha Wananch CUF mpaka pale shauri la msingi
litakaposikilizwa.
“Mh
Spika anapaswa, kuzingatia kwa busara uamuzi uliotolewa na mahakama kwa
kuwaondoa wale Wabunge wa Lipumba ndani ya Bunge na kuwarejesha Wabunge
halali sasa, Mpaka hapo haki itakaposhinda zaidi,”ameandika Lema
Wabunge
hao nane walivuliwa uanachama Julai 24 na Baraza Kuu la Uongozi la
Taifa la Chama cha Wananchi, CUF linaloongozwa na Prof. Lipumba kwa
madai ya utovu wa nidhamu yakiwemo kukisaliti chama hicho.
chanzo:mpekuziblog.
Comments