Katibu Mkuu CHADEMA Atoa Neno Uchaguzi Mdogo wa Madiwani.....Azungumzia Sakata la Wanaohamia CHADEMA.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Vincent
Mashinji amesema kuwa baadhi ya wasimamizi wa Uchaguzi mdogo wa udiwani
ambao unatarajiwa kufanyika karibuni katika Kata 48 katika mikoa 18
nchini wamepewa maelekezo kutowatangaza Madiwani CHADEMA wakishinda.
Ameyasema
hayo leo kupitia mtandao wake wa Twitter na kudai kuwa hiyo itakuwa ni
fursa kwao wao CHADEMA kuwaonyesha na kuwafundisha ustaarabu mpya ambao
wameuanzisha.
“Wasimamizi
wa uchaguzi wana maagizo ya kutowatangaza madiwani wa CHADEMA watakao
shinda. Hii ni fursa kwetu kuwafundisha ustaarabu mpya. Na imani maneno
haya utayakumbuka nikupe mshahara, nyumba na gari halafu umtangaze
mpinzani kashinda,”amesema Mashinji
Aidha,
mbali na hilo Mashinji amejibu hoja ya Rais ambayo aliitoa akiwa Mwanza
kuwa wezi ambao walikuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walikimbilia CHADEMA
na kudai kuwa watu hao ambao wanatoka CCM na kwenda CHADEMA wameamua
kuokoka.
Hata
hivyo, ameongeza kuwa kuhama kwa wanachama kutoka Chama cha Mapinduzi
CCM kwenda Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa wameokoka
hivyo wameenda sehemu sahihi.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments