Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana imetakiwa kufutilia vyanzo vyao vya mapato ikiwemo Mashamba ya kilimo ili waweze kujitatulia mahitaji yao pamoja na kusaidia jamii katika miradi ya maendeleo.
Akizungumza katika Uzinduzi wa Bodi mpya ya kamisheni hiyo Mazizi ,Waziri wa Nchi Ofisi ya raisi Katiba, Sheria ,Utumishi wa Umma na utawala bora Haroun Ali Suleiman amesema kamisheni hiyo itakapofuatilia vizuri vyanzo vyao wataweza kuzalisha mapato yatakayoisaidia jamii.
Amesema jamii imekabiliwa na matatizo mengi ikiwemo uhaba wa huduma ya maji safi na salama pamoja na Uhaba wa Fedha za ujenzi wa madrasa katika jamii hivyo mapato yatayopaikana yatasaidia kuwawezesha wananchi kuyapatia ufumbuzi matatizo yanayowakabili.
Amesema mbali na migogo inayojitokeza katika usimamizi wa mashamba ya kilimo yanayosimamiwa na kamisheni hiyo wasivunjike moyo badala yake waendee kufanya kazi kwa kufuata sheria na maadili ili waweze kuwasaidia wananchi hususan wenye kipato cha chini.

Aidha Waziri Harouna ametowa wito kwa bodi hiyo mpya kufuatilima mali zote za kamisheni hiyo ikiwemo Nyumba Na Mashamba ya kilimo ili yaweze kuwanufaisha wananchi kisheria.
’’Bodi hii mpya nataka iwe na takwimu za kutosha za kutambua mali zetu zote zilipo na nani anatumia mali hizo na katika mali zilizokodishwa je zipo salama kama hazipo salama zirejeshe katika mikono ya Kamisheni’’
Kwa upande Mwenyekiti aliemaliza Muda wake katika Bodi hiyo Issa haji Zidi amesema licha ya utekelezaji wa majukumu yao lakini wamekabiliwa na matatizo mbali ikiwemo uhaba wa bajeti ya kujiendeleza katika utendaji wa shughuli zao na kutowa wito kwa serikali kuangalia namna ya kuwarejeshea mashamba ya wakfu waliyokuwa nayo awali.
Nae wake Mwenyekiti Alieteuliwa kuongoza Bodi hiyo Prof.Hemed Rashid Hikman amesema watahakikisah wanasimamia ipasavyo wajukumu yao katika kuleta maendeleo nchini pamoja na kuimarisha ushirikano kwa watendaji wa bodi hiyo katika kuisadia jamii hususani watu wenye kipato cha chini.
chanzo:Zanzibar24.
Comments