
Hatua hiyo imekuja kufuatia pendekezo lililotolewa na Rais John
Magufuli Novemba 25 aliyetaka hospitali hizo zitolewe TAMISEMI ziwe
chini ya Wizara ya Afya ili kuweza kuwapo kwa mfanano wa sera lakini pia
ugawaji wa rasilimali watu katika hospitali hizo.
Rais aliyasema hayo alipokuwa akizindua Hospitali ya Taaluma na Tiba
ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Kampasi
ya Mloganzila na kueleza kuwa kumekuwa na utofati mkubwa wa ugawaji wa
madaktari katika hospitali za rufaa kutokana na mgawanyo huo kufanywa na
wizara mbili tofauti.
Mbali na Rais kuagiza hospitali hizo ziwe chini ya Wizara ya Afya ili
zisimamiwe vizuri na wataalamu na pia ameiagiza wizara hiyo kurekebisha
mgawanyo wa madaktari katika hospitali zote nchini ili kuepuka uwepo
madaktari wengi katika sehemu moja, huku maeneo mengine yakiwa na uhaba
mkubwa.
“Kuanzia leo (Novemba 27) hospitali zote za rufaa
zitakuwa chini ya Wizara ya Afya na kwetu sisi (TAMISEMI) tutabaki na
hospitali za wilaya, vituo vya afya na zahanati pekee,” amesema Waziri Jafo.
Kuhusu madaraka ya Waganga Wakuu wa Mikoa amesema wataendelea kuwa
chini ya TAMISEMI lakini Waganga Wafawidhi wa Hospitali watapelekwa
Wizara ya Afya.
chanzo: zanzibar24.
Comments