Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) chakumbwa na jeraha kwa kuondokewa na wanachama 50 mkoani Geita ambao wamehamia Chama cha Mapinduzi (CCM) wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Katibu wa UVCCM wilayani Geita Bw. Ali Rajab alisema vijana hao 50 kutoka kijiji cha Buligi kata ya Senga wilayani Geita wamehama Chadema na kujiunga na CCM kutokana na kasi ya utendaji ya Rais Magufuli.
Katika kampeni hizo Bw. Rajab amewataka watumishi kuacha kufanya kazi kwa mazoea ili kuendana na kasi ya Rais Magufuli na Chama cha Mapinduzi CCM kwa ujumla.
Naye Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa wanawake, UWT wilayani Geita Bi. Mazoea Salim, amesema CCM inatarajia kushinda kwenye uchaguzi huo mdogo katika kata ya Senga kutokana na uwezo wa mgombea ambaye wamemsimamisha.
chanzo:zanzibar24.
Comments