Bwana harusi ajeruhiwa vibaya sehemu za siri, kwenye nyonga na mkononi baada ya kupigwa na risasi iliyokuwa imelengwa kufyatuliwa juu hewani kama ishara ya kusherehekea harusi yake.
Tukio hilo limetokea huko nchini Misri ambapo Osman al-Alsaied mwenye umri wa miaka 28 alikuwa akisherehekea usiku wake wa mwisho akiwa kapera wakati silaha hiyo ilipofyutuliwa upande wake badala ya hewani.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa bunduki hiyo ilifyatuliwa kiuzembe na mwanamume mwenye umri wa miaka 26.
Wanasema kuwa alitoroka muda mfupi baadaye baada ya kisa hicho lakini akakamatwa na sasa anahojiwa.
Ripoti za kisa hicho zimechochea hisia kali katika mtandao wa kijamii huku wengi wakitaka sherehe za aina kama hiyo ya kufyatua risasi hewani kusitishwa zisifanyike tena.
Iwapo unafyatua risasi wakati unasherehekea furaha yako je itakuwaje wakati unapokasirika, ujumbe mmoja wa Twitter uliuliza.
Kulikuwa na kisa kama hicho katika harusi nchini Misri mwezi uliopita kulingana na mtandao wa Stepfeed.
Katika kisa hicho bwana harusi alifanyiwa upasuaji na matibabu baada ya risasi kumpiga katika nyonga yake.
chanzo:zanzibar24.
Comments