
Sanjiv Kumar mwenye umri wa miaka 35 alidaiwa kumyonga mkewe ,Suman wakati wa vita siku ya Jumanne.
Mwanamume huyo alikiri kutekeleza kitendo hicho baada ya kukamatwa , afisa wa polisi Ramesh Jaglan aliambia BBC.
Migogoro ya kinyumba ndio yenye visa vingi vilivyoripotiwa dhidi ya wanawake nchini India kwa zaidi ya muongo mmoja sasa.
”Alikuwa akikataa kufanya ngono kwa muda .Siku ya Jumanne alikataa tena, hatua iliomuudhi na kuamua kumnyonga.Tumemkamata”, bwana Jaglan aliambia BBC.
Wanandoa hao walikuwa wameoana kwa zaidi ya muongo mmoja na Wana watoto wawili.
chanzo: zanzibar24.
Comments