
Akamatwa na kuhemea katika Hospitali ya kivunge kwa matibabu baada ya
kujifungua huku akiwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa
Kaskazini Unguja, wakati kichanga hicho kimeshapelekwa nyumba ya
kulelewa watoto mazizini.
Akithibitishwa kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo Kaimu Kamanda Mkoa wa
Kaskazini Unguja Suleiman Hassan Suleiman amesema mtuhumiwa huyo mwenye
umri wa miaka 16 amaekamatwa wakati amekimbilia hospitali ya kivunge kwa
matibabu baada ya hali yake kuwa mbaya baada ya kujifungua.
Kaimu Kamana huyo amesema kuwa msichana huyo amejifungua kwa
kujificha na baadae kumtelekeza mototo jaani kwani ni kitendo ambacho ni
cha kusikitisha sana.
Amesema mpaka sasa mtuhumiwa huyo yupo chini ya ulinzi wakati
amelazwa hospitali ya kivunge kwa matibabu na baada yahapo hatua za
kisheria zitachukuliwa juu yake.
chanzo:zanzibar24.
Comments