Wenye kuuza miili yao wapo hatarini Kaskazini Unguja.

Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini A Unguja limetakiwa kuongeza nguvu zaidi katika kuwadhibiti wanawake wanaofanya biashara ya kuunza miili yao katika kijiji cha Nungwi.

Akizungumza na Zanzibar24 Mkurugenzi wa halmashauri ya kaskazini A Mussa Ali Makame amesema hatua hiyo itaweza kusaidia kupunguza vitendo hivyo ambavyo vimekuwa vikiathiri jamii na kuporomosha maadili.

Amesema kuna baadhi ya wananchi wanachangia kuwepo kwa vitendo hivyo kwakuwakodisha watu wanaofanya biashara hiyo nyumba zao jambo ambalo linasababisha kuongeza kwa biashara hiyo siku hadi siku katika maeneo ya nungwi licha ya kuwa serikali inakataza vitendo hivyo.
Hata hivyo amefahamisha kuwa tayari halmashauri imefanya operesheni na kufanikiwa kuwakamata wanawake kumi wanaofanya biashara ya kuuza miili yao na kuwafikisha katika vyombo vya sheria na kuahidi zoezi hilo litakuwaendelevu ili lengo la serikali la kudhibiti vitendo hivyo lifikiwe.
Aidha Mussa amesema halmashauri hiyo imeweka mikakati madhubuti ya kufanya doria za usiku ili kutokomeza kabisa vitendo hivyo na kuwataka wananchi kutoa taarifa pindi watakapo gundua kuna nyumba inafanywa biashara hizo haramu ambazo zipo kinyume na sheria.
chanzo:zanzibar24.

Comments