Waziri
wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba leo mchana (Oktoba 17) amekagua
eneo la ujenzi wa nyumba za Polisi jijini Arusha zinazoendelea kujengwa
baada ya ajali ya moto iliyotokea mwishoni mwa mwezi Septemba ambayo
ilisababisha familia za askari 13 kuunguliwa vitu mbalimbali na kukosa
makazi.
Mwigulu
alitumia fursa hiyo kwa kuishukuru kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa
ambayo inaoongozwa na Mkuu wa mkoa Mh. Mrisho Gambo lakini pia
aliwashukuru wadau ambao wote kwa pamoja walichukua hatua za haraka za
kurejesha makazi ya askari ambao walikumbwa na janga la moto huku
akisisitiza kwa kusema kwamba hali ilioonyeshwa na wadau hao ni mfano
mzuri wa kuigwa na mikoa mingine waone nchi inajengwa na wananchi.
Alisema
kwamba suala la makazi ya askari lipo katika kipaumbele cha serikali na
Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameonyesha kwa vitendo
katika maeneo tofauti ikiwemo hapa Arusha.
Alisema
Serikali ikishamaliza hilo itaendelea na utaratibu mwingine wa kujenga
majengo ya kisasa ili askari wapate makazi bora huku akimuagiza Kamanda
wa Polisi mkoa wa Arusha awafikishie salamu askari wa Arusha kwamba, Mh.
Rais yupo pamoja nao na Wizara ipo pamoja nao.
Naye
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo
mbali na kuendelea kuwashukuru wadau hao kwa kujitolea na kumuunga mkono
Mh. Rais ambaye alionyesha njia siku hiyo hiyo usiku kabla
hakujapambazuka kwa kutoa mchango wake kama Serikali, lakini pia alisema
bado milango ipo wazi kwa watu wengine ambao hawakuwa na taarifa juu ya
tukio hilo ili kulisaidia Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha liweze
kufanikisha ujenzi wa makazi ya askari hao.
Kamanda
Mkumbo aliongeza kwa kusema ujenzi wa makazi bora ya askari mkoani hapa
utasaidia kuwaongezea morali zaidi wa kazi askari hao hali ambayo
itazidi kuimarisha usalama na shughuli za maendeleo kusonga mbele.
Jumla
ya nyumba 29 za askari katika moja ya kambi iliyoathirika na ajali ya
moto zilianzwa kujengwa toka tarehe 2 mwezi huu jijini hapa na saba
ambazo zipo katika ngazi ya msingi zinatarajiwa kujengwa katika kituo
kidogo cha Polisi Morombo kata ya Murieti.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments