
Awali kupitia ukurasa wake wa Twitter Mbunge Ally Saleh alimlaumu
Waziri Makamba kuwa amekuja Zanzibar kushughulikia kero za Muungano
lakini yeye kama Waziri kivuli hakujua chochote kwa kutofahamishwa
kuhusu ujio huo.
Nae Waziri Makamba kupitia mtandao huohuo wa Twitter alimjibu Waziri
Makamba kuwa itakua vigumu kwa kila Waziri anapofanya kazi kumjulisha
Waziri kivuli lakini alitumia nafasi hiyo kukiri kughafilika kwake
kumjulisha Mbunge huyo kama rafiki na mdau wa mambo ya muungano.
Waziri Makamba yupo katika ziara ya kikazi visiwani hapa kwa muda wa
siku saba akiwa amejikita zaidi kushughulikia masuala ya uchumi ikiwa ni
pamoja na masuala ya Bandari, Forodha, Kodi na kubaini changamoto
zilizopo, utekelezaji wa maazimio yaliyokubaliwa katika vikao vya
majadiliano na kuangalia maeneo mapya yanayohitaji kuingizwa katika
mfumo wa utatuzi.
Comments