
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, walisema mkombozi wa kweli
wanaemfikiria ndani ya baraza lao, sio jambo jengine, bali ni kupatiwa
mashine hiyo, ambayo wanaamini haina msimu.
Walisema kutokana na kuanza kupoteza nguvu za kuendeleza kilimo,
inakuwa ni vigumu kuwa na miradi inayohitajika kutumia nguvu, bali
miradi ya aina hiyo, ndio wanayoimudu.
Katibu wa baraza hilo Ali Juma Khamis, alisema wanaamini kuanzishwa
kwa mabaraza hayo, yanayolelewa na JUWAZA na Help Age International
Tanzania, kunaweza kuwakomboa, hasa wakiwa na miradi.

Alisema jamii imekuwa ikiwapa kisogo wazee kwa kutowapatia huduma
kamili, kama walivyobinadamu wengine, na ndio maana baada ya kujikusanya
pamoja ndani ya mabaraza hayo, yanaweza kuwanawirisha.
“Sisi kulima hatuna nguvu tena, lakini kama wafadhili au hata
serikali yetu itatupatia mashine kama ya kusagia nafaka, basi
tutajiongezea kipato na kuondokana na utegemezi ndani ya familia zetu”,alisema.
Nae mshika fedha wa baraza hilo Jine Ali Abeid, alisema aina yoyote
ya miradi, ambayo haihitaji kutumia nguvu sana, inaweza kuwasaidia
kujikomboa.
“Hata kama tukipata miradi kama ya ufugaji, biashara ndogo
ndogo kwa mujibu mazingira yetu, sisi tunaamini kwa umoja wetu, basi
tutafikia pahala pazuri”,alisema.

Kwa upande wake mjumbe wa baraza hilo la wazee shehia ya Vitongoji
Ali Omar Abdalla, alisema waliamua ,kujikusanya pamoja ili wawe na sauti
moja, ya kutetea haki zao.
Alisema, wazee wanamahitaji kadhaa ikiwa ni pamoja na matibabu kuwa
na dirisha pekee la dawa, kwenye vyombo vya usafiri kutokaa foleni, haki
ambazo wasipokaa pamoja ni vigumu kutekelezwa.
“Wazee wa shehia hii ambao bado hawajajiunga, muda ndio huu,
maana wakikaa pembeni na kisha kudai haki zao inakuwa vigumu kuzipata”,alisema.

Kwa upande wake mlezi wa bara hilo, ambae ni sheha wa shehia hiyo
Salim Ayoub Suleima, alisema kutokana na idadi ya wazee 180 walio na
umri wa kuanzia miaka 6o na kundelea bado baraza hilo ni dogo.
Alisema wazee wa shehia yake, wanakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwa
ni pamoja na waliofika umri wa miaka 70 kutopata pencheni jamii, kwa
vile hukosa msimazi wa ndani ya shehia yake.
“Naamini wazee hawa wa Vitongoji, sasa kama wakikaa pamoja
hakutakuwa na mzee ambae anastahiki kupewa pencheni jamii kukosa, maana
itakuwa wanamfuatiliaji”,alieleza.
Mapema Mratibu wa mabaraza ya wazee kisiwani Pemba kutoka JUWAZA,
Sifuni Ali Haji, alisema waliamua kuwashawisha wazee, kuanzisha mabaraza
hayo, ili wapate kutetea haki zao wakiwa pamoja.
Alifafanua kuwa, wazee wa Zanzibar kama walivyowazee wengine duniani
kote, wanazo haki zao mbali mbali ikiwemo wa matibabu, mitaji na kutoa
maoni yao katika kuendesha nchi, hivyo kupitia mabaraza hayo itakuwa
rahisi.
“Mabaraza haya ya wazee yana malengo mbali mbali, na kama
wenyewe wakiyaendelea yanaweza kupiga hatua kubwa, huku na sisi JUWAZA
tukiwa bega kwa bega nayo”,alifafanua.
Shehia ya Vitongoji wilaya ya Chakechake kisiwani Pemba, ina wazee
173 wenye umri wa miaka 70, na wazee 180 wenye umri wa kuwanzia miaka 60
hadi 69, ambapo baraza hilo la wazee lililoanzishwa mwaka jana
linawanachama 15.
Katika ziara hiyo ilioratibiwa na Jumuia ya wazee Zanzibar JUWAZA,
ilianzia shehia ya Wingwi mapofu na kumalizia shehia ya Vitongoji.
chanzo:zanzibar24.
Comments