
Hayo ameyasema huko katika ofisi zao zilizopo Maisara wakati akitoa
ripoti kwa waandishi wa habari kuhusu uvumi uliojitokeza nchini wa
upungufu wa huduma hiyo.
Alisema kuwa kwa sasa Zanzibar mafuta yapo ya kutosha lita Milion 1.
7 za Petrol zipo na kwa siku zaidi ya lita 165,000 ya petrol ni
mahitaji ya matumizi ya mafuta,na idadi hiyo inaweza kutosheleza zaidi
kwa matumizi Zanzibar kwa siku kumi na moja.
Aidha aliwatoa hofu wananchi kwa kusema kuwa meli ya mafuta ipo
njiani baada ya siku 4 itaingia nchini na kushusha mafuta ya kutosha.
“ Serikali inasimamia vyema kuhakikisha mapungufu haya
hayaendelei na kuwathibitishia wananchi mafuta yapo ya kutosha na bei
zile zile zilizokuwepo kama kawaida”Alisema kaimu huyo.
Aidha amewataka wananchi waache kununua mafuta kwa njia ya magendo
ili kuuza kwa bei iliyokuwa si halali ambayo imethibitishwa na Serikali.
chanzo: zanzibar24.
Comments