
Walisema hutuba hiyo ni miongoni mwa hutuba kadhaa zinazotolewa na
rais huyo na kuibua hisia, mawazo mapya ndani ya jamii, jambo ambalo
huwazidisha upendo kwa kiongozi wao.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu, baadhi ya
wananchi hao walisema, hutuba hiyo ilikuwa imejaa kila aina ya utendaji,
utekelezaji, ahadi na mafanikio yaliopo ndani ya serikali anayoiongoza.
Mmoja kati ya wananchi hao, Abdull-hamid Juma Makame wa Mchanga mdogo
wilaya ya Wete, alisema yeye kwenye hutuba hiyo, lililomvutia ni pale
rais alipotangaza kufuta michango ya elimu ya sekondari.
Alisema tamko hilo kwake, limempa hisia mpya kwamba rais huyo amekuwa
akiwajali wanyonge wa nchi hii, kwa lengo la kuona watoto wote,
wanapata elimu bila ya kujali uwezo wa wazazi na walezi wao.
Nae Mashavu Himid Mbaruok wa Wingwi mapofu wilaya ya Micheweni,
alisema mara zote rais huyo wa Zanzibar anapotoa hutuba kwenye sherehe
mbali mbali za kitaifa, hulenga kuwapatia wananchi huduma sawa.
“Mimi sikutarajia kuwa, kwa vile ameshafuta michango ya
elimu ya msingi mwaka jana, na atangaaze kufuta michango ya sekondari,
lakini amefanifaya na mimi kama mazazi mwenye watoto wanne mwakani
wanaoingia sekondari napongeza”,alifafanua.
Hata hivyo Muhidini Ameir Ali wa Machomane Chakechake, alisema
hutuba hiyo ya rais aliyoitoa Septemba 23, inafaa kuandikiwa kitabu
chake maalum, ili ihifadhiwe na ije isomwe na vizazi vijavyo.
Alisema hutuba hiyo ya rais ilieleza historia ya kielimu Zanzibar
kabla na baada ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964, ambayo
skulini haisomeshwi.
“Mimi kwenye hutuba ile ya rais, nililoliona kwangu ni
kubwa na inafaa kuwekewa kumbu kumbu, ni suala la historia ya elimu, na
sasa ndani ya awamu hii ya saba ilivyoimarishwa”,alieleza.
Kwa upande wake Habiba Mjaka Kombo wa Mtambile, alisema kilichomvutia
yeye kwenye hutuba ya rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la
Mapinduzi Mhe: Dk Ali Mohamed Shein, ni ahadi ya kujenga skuli tisa za
ghorofa Unguja na Pemba.
Aidha alisema jengine lililomvutia ni kuona jinsi rais alivyotekeleza
upanuzi wa skuli 23 na nyengine kufanyiwa matengenezo makubwa, ununuzi
wa vifaa vya maabara na samani.
Mwenyekiti wa masheha wilaya ya Micheweni Dawa Juma Mashindo, alisema
yeye alivutiwa na kila jambo, ingawa rais kutangaaza kipaumbele cha
kutanua elimu kilimkosha roho.
Septemba 23, mwaka huu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe: dk Ali Mohamed Shein, alikamilisha kilelele cha
maadhimisho ya siku ya elimu bila ya malipo, uwanja wa Gombani kwa
hutuba yake, alioeleza mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na kutangaaza
kufuta michago ya elimu ya sekondari.
chanzo: zanzibar24.
Comments