UNESCO yatoa mwanya wa ukarabati kwa Hotel ya Bwawani.

Jengo la Hotel ya Bwawani linatarajiwa kuanza ukarabati baada ya kufanyika tathmini ya Mazingira pamoja na kupatikana kwa kibali cha Urithi wa Mji Mkongwe kutoka UNESCO.

Akijibu Swali katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar Waziri wa fedha na Mipango Dk. Khalid Salum amesema ni kweli kwa muda Mrefu jengo hilo halijaendelezwa lakini hatua za awali za uendelezaji wa Jengo hilo umenza.


Amesema maafisa kutoka UNESCO tayari wapo nchini kwa ajili ya ukaguzi wa miradi iliopo katika Maeneo mbali mbali ya Urithi wa Mji mkongwe ikiwemo Jengo la Hoteli ya Bwawani , Bet al jaib na koridoo za darajani ili kuzipatia vibali vya kuendeleza majengo hayo.

Akizungumzia sababu za kuchelewa kwa jengo hilo Dk. Khalid amesema ni pamoja na kutokamilika kwa wakati kwa tathmini za kimazingira kumechangia kuchelewa kwa ujenzi huo.

Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea na jitihada za kumharakisha muekezaji ili ukarabati huo uweze kukamilika kwa wakati katika kuimarisha maendeleo Nchini.

Hoteli hiyo imekodishwa kwa kampuni ya Quality Group ya Dar es Salaam november 17 -2015 .

chanzo:Zanzibar24.

Comments