Uchaguzi wa marudio wa urais Kenya katika kaunti nne waakhirishwa hadi kesho.

Uchaguzi wa marudio wa urais Kenya katika kaunti nne waakhirishwa hadi kesho
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) imetangaza kuwa zoezi la upigaji kura lilikwamishwa jana katika baadhi ya maeneo kutokana na changamoto za kiusalama na kwamba zoezi hilo litafanyika kesho Oktoba 28.


Wakati huo huo taarifa zinaeleza kuwa mkoa wa Pwani nchini Kenya umeshuhudia kiwango cha chini cha wapiga kura baada ya watu wengi kususia uchaguzi huo wa marudio wa urais jana Alhamisi.

Muungano wa upinzani (Nasa) umewahimiza wafuasi wake kutoshiriki uchaguzi huo baada ya kiongozi wa muungano huo Raila Odinga kujiondoa katika kinyang'anyiro hicho. 
Miito iliyotolewa na Raila ya kususia uchaguzi huo wa jana inaonekana kuitikiwa katika kaunti zote za Mombasa, Kwale, Kilifi, Taita Taveta, Tana River na Lamu japokuwa baadhi ya watu walijitokeza katika vituo vichache vya kupigia kura katika maeneo ya magharibi mwa Lamu.

Hadi tunaingia mitamboni Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee alikuwa akiongoza kwa kupata kura 2,414, 839 huku mpinzani wake, Raila Odinga wa NASA aliyesusia zoezi hilo akiwa na kura 27 elfu 529. 
chanzo: parstoday.

Comments