
“Bw Lissu ametolewa katika chumba cha wagonjwa mahututi na kuwekwa
katika wodi ya kawaida huku akiwa na uwezo kamili wa kuongea na kutembea
kwa kutumia kiti cha magurudumu,” alifafanua Mbowe. Hata hivyo, Chadema
imesema kuwa, kwa kuhofia usalama wa Lissu, kwa sasa hawatamrudisha
nchini Tanzania.
“‘Kwa sababu za kiusalama hatutaweza kusema atakwenda wapi lakini
itoshe tu kuwaambia kuwa ataanza awamu ya tatu ya matibabu nchi
nyingine, sio Tanzania wala sio jirani”.
Tundu Lissu alipigwa risasi zaidi ya thelathini na watu ambao mpaka
sasa hawafahamiki mwanzoni mwa mwezi uliopita huko mjini Dodoma
alipokuwa akihudhuria vikao vya bunge. Hivi karibuni, ndugu zake Bw
Lissu wameitaka serikali kuvishirikisha vyombo vya upelelezi vya
kimataifa kama vinavyoshirikishwa katika mambo mengine ili kuongeza
ufanisi katika upelelezi huo.
Jeshi la polisi nalo limeomba lipewe nafasi wa kufanya
upelelezi.Tundu Lissu yuko nchini Kenya kwa takribani wiki nne sasa kwa
ajili ya matibabu.
chanzo: zanzibar24.
Comments