
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa, Dkt. Agnes Kijazi ameeleza
hayo jana na kusema kuwa katika kipindi hicho kunatarajiwa kuwa na
vipindi vifupi vya mvua kubwa katika maeneo mbalimbali nchini ambavyo
vinaweza kusababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo.
Dkt. Kijazi amewataka wanajamii na wadau wa sekta mbalimbali
zinazohusiana na mazingira kufuatilia kwa ukaribu taarifa za hali ya
hewa zinazotolewa ili kuondokana na madhara yanayoweza kuepukika.
“Wadau wa sekta ya uvuvi, kilimo, mifugo, chakula na
wanyamapori wanatakiwa kufuatilia kwa ukaribu taarifa za hali ya hewa.
Kufahamu mapema kutasaidia kujipanga,” alisema Dkt. Kijazi.
Aliongeza kuwa kufuatia mvua hizo zinazotarajiwa, kiwango cha unyevu
katika udongo kitaongezeka na hivyo kuwataka wachimbaji wadogo wa madini
kuchukua tahadhari kwani unyevu huo unaweza kupelekea mmomonyoko wa
ardhi na kuleta maafa.
Aidha, amezitaka mamlaka za miji na sekta mbalimbali kuhakikisha
wanafanya ukaguzi wa mitaro na mifereji ya kupitisha maji iwe inafanya
kazi muda wote ili kuepusha kutuama kwa maji na kusababisha mafuriko
pamoja na maonjwa ya milipuko.
“Sekta ya afya ichukue hatua stahiki ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza kutokana na vipindi vifupi vya mvua kubwa vinavyoweza kusababisha milipuko ya magonjwa,” amesema Dk.
chanzo: zanzibar24.
Comments