Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kuwa Awamu ya Pili ya Udahili wa waombaji wanaotarajiwa kujiunga na masomo ya shahada za awali ulimalizika tarehe 10 Oktoba 2017. Kutokana na waombaji wengi kutochaguliwa kwa sababu mbali mbali, tume imesema itafungua maombi kwa Awamu ya Tatu kuanzia tarehe 18 hadi 22 Oktoba 2017 na siyo 16 hadi 18 ya awali.
Katika taarifa ya TCU wamesisitiza kuwa, awamu hii itawahusu waombaji waliokosa nafasi kwenye Awamu ya Kwanza na
ya Pili kutokana na ushindani au kukosa sifa katika programu walizoomba, waombaji waliochaguliwa zaidi ya chuo kimoja; wanatakiwa kuamua mara mojakwa kuchagua chuo kimoja tu na hatimaye kukiarifu chuo husika, awamu hii haitawahusu waombaji wapya (ambao hawajawahi kutuma maombi katika awamu mbili zilizopita) na pia waombaji ambao hawatathibitisha uchaguzi wao au kujithibitisha zaidi ya chuo kimoja hawatatambuliwa na Tume katika udahili wa mwaka 2017/18.
Aidha, wameendelea kusisitiza kwamba, waombaji kuwasiliana moja kwa moja na mara kwa mara na vyuo husika kwa
masuala yote yanayohusiana na zoezi la udahili badala ya kuja TCU na pia, waombaji wote kutembelea Tovuti za vyuo ili kufahamu hatima ya maombi yao.
Pia, Tume inapenda kusisitiza kuwa utaratibu wa kutuma maombi na kuthibitisha ni ule ule uliotumika katika awamu mbili zilizopita za udahili.
chanzo:zanzibar24.
Comments