
Hayo yamesemwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai wakati akifanya mahojiano na kituo cha Azam.
Spika Ndugai alisema ingekuwa vizuri kama kiongozi Lazaro Nyalandu angewasilisha kwanza barua hiyo katika ofisi ya spika kabla ya kwenda kutoa taarifa kwa vyombo vya habari.
Alipoulizwa kuhusu hatua atakayoichukua baada ya kupokea barua ya
Nyalandu, Ndugai alisema kwamba, kwa sasa hawezi kuzungumzia kitu
ambacho hakijatokea, lakini endapo atapokea barua hiyo, na Nyalandu
akathibitisha kwamba ni ya kwake, basi wataweza kukaa kujadili uamuzi
huo.
Katika taarifa yake ya asubuhi, Nyalandu alisema kuwa, amemuandikia
Spika Ndugai barua ya kujiuzulu Ubunge ambao ameutumikia tangu mwaka
2000.
“…asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job
Ndugai, Mb., barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya UBUNGE wa Jimbo la
Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa
vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo
mwaka 2000 hadi Sasa.”
chanzo: zanzibar24.
Comments