
Mwenyekiti wa taasisi hiyo Salim Mussa Omar amekabidhi msaada huo kwa wanafunzi na kuiomba jamii na wadau wa elimu nchini kuwakumbuka wanafunzi kwa kuwasaidia ili kuwarahisishia kielimu.

Aidha mwenyekiti huyo amesema, “Huwezi kujenga jamii imara bila kuweza kuweka misingi ya elimu vizuri hatuwezi kuwa na taifa lililoendelea bila ya kuwa na vijana waliondelea kielimu” .
Nao baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wameishukuru taasisi hiyo na kusema kuwa kufanya hivyo imeonesha ni jinsi gani jamii ianavyowajali, na kuomba wadau waendelee kuwapa misaada ili kuwapunguzia baadhi ya changamoto zinazowakabili.
chanzo:zanzibar24.
Comments