Rais
Dk. John Magufuli amesema mkuu wa mkoa yoyote atakayeshindwa kupeleka
wawekezaji kujenga viwanda katika mkoa wake hatamvumilia.
Amewataka
wakuu wote wa mikoa kuiga mfano wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John
Mongella, ambaye amekaribisha wawekezaji wanaojenga viwanda vipya.
Agizo hilo alilitoa Mwanza jana alipokuwa akituhubia mkutano wa hadhara eneo la Nyakato wilayani Ilemela.
Rais alisema viwanda si mali yake bali ni mali ya wananchi ambao ndiyo walipa kodi.
Alisema
ingawa Tanzania ilikuwa na viwanda vingi, hivi sasa Watanzania
wamebaki hawapati majibu vilikwenda wapi hali inayoifanya Serikali
iamue kufanya kazi ya kuvifufua vya zamani na kujenga vipya.
Kabla
ya kuhutubia mkutano huo Rais alizindua kiwanda cha vinywaji baridi
cha Sayona kilichojengwa Nyakato. Leo anatarajiwa kuzindua viwanda
vingine viwili.
Alisema
amefurahishwa na ahadi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela na
kwamba kila anapopita ndani ya mkoa huo, lazima huzindua kiwanda ama
viwanda kwa vile wawekezaji wengi hukimbilia kuwekeza mkoani humo.
“Nataka nichukue fursa hii kukupongeza mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa kuwatafuta wawekezaji wengi na kuwekeza kwenye viwanda.
“Nataka
wakuu wa mikoa wa aina hii, mkuu wa mkoa ambaye kila siku napita mkoa
wake bila kuzindua kiwanda sitamvumilia kufanya naye kazi, lazima
ang’oke.
“Mkuu
wa Mkoa ambaye haleti wawekezaji katika mkoa wake kujenga viwanda…
kwanza hivyo viwanda si vya wakuu wa mikoa bali ni mali ya wananchi.
Kuwapo viwanda kutasaidia kutengeneza ajira, hayo ndiyo maendeleo
tunayotaka.
“Haiwezekani Tanzania iwauzie … tulime pamba tuwauzie wazungu watengeneze nguo wazivae kisha kutuletea zikiwa mitumba.
“Tunataka
nguo zitengenezwe hapa na Mwatex ili ziuzwe kwa bei nafuu kuliko hiyo
mitumba. Sizuii mitumba lakini nguo mpya na bora lazima zitengenezwe
hapa,” alisema Rais Magufuli.
Alimweleza
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage,
ajirekebisha na afanye kazi ya kufufua, kufunga na kuchukua viwanda
visivyofanya kazi na awape watu wengine.
“Haiwezekani
unapewa kiwanda kutoka mwaka wa kwanza hadi wa 20 bila uzalishaji,
wenye viwanda hivyo virudisheni haraka kwa sababu tutakapoanza
kuwashika tutadai faida ambayo walikuwa wakiipata miaka hiyo,” alisema.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments