
Polisi wanachunguza mashambulizi kwenye nyumba za Bobi Wine ambaye
jina lake kamili ni Robert Kyagulanyi, anayewakilisha eneo la Kyaddondo
West na Allan Ssewanya ambaye ni mbunge wa Makindye West.
Mashambulizi hayo yalifanyika mapema Jumanne.
Wiki iliyopita shambulizi liliripotiwa kwenye nyumba ya mbunge mwingine Moses Kasibante ambaye ni mbunge wa Rubaga North.
Kwenye ujumbe kupitia mtandao wa Facebook, Bobi Wine alisema kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa nyumbani kwake.
Amesema amekuwa akipokea vitisho vya kuuliwa karibu kila siku.
Gazeti la New Vision lilisema kuwa wabunge ambao nyumba zao
zilishambuliwa ni baadhi ya wale waliotimuliwa bungeni kufuatia ghasia
wakati wa mijadala kuhusu kuondolewa kwa umri wa kuwania urais.
chanzo: zanzibar24.
Comments