Waziri
wa Habari, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amefunguka na kusema kuwa Mzee
Majuto amedhurumiwa pesa milioni 25 na kampuni ya filamu ambayo jina
lake amelihifadhi na kudai atatumia hata mshahara wake kuhakikisha
anawafunga watu hao.
Mwakyembe
amesema hayo leo Oktoba 27, 2017 alipokutana na wasanii mbalimbali
kujadili changamoto za kazi ya sanaa nchini na kusema katika vitu
ambavyo atapambana navyo ni pamoja na watu wanaowadhurumu wasanii haki
yao na kuwaibia kazi zao za sanaa.
"Nilipopita
Tanga nilikutana msanii nguli wa filamu Mzee Majuto nilikwenda kumjulia
hali na bahati nzuri saizi anaendelea vizuri, Mzee Majuto akaniomba
kitu kimoja na kuniambia naumwa nahitaji pesa lakini nimeshafanya kazi
na kampuni hii akanionyesha na kuwa ameshatengeneza filamu zaidi ya 100
na kampuni hiyo kwa mkataba wa kulipwa fedha ndogo tu shilingi milioni
25 lakini huu ni mwaka wa pili hajalipwa hata senti tano sasa hayo
ndiyo mambo ambayo sifurahii, nimeshapeleka taarifa kwa hiyo kampuni
tukutane Dar es Salaam na Dodoma asipokuja tunajua njia za kumsafirisha
kwenye kalandinga mpaka Dodoma, huu ni wizi kama wizi wa kwenda
kumchomolea mtu mfukoni" alisisitiza Mwakyembe
Waziri
Mwakyembe aliendelea kufafanua kuwa kwa sasa yupo tayari kutumia pesa
zake mfukoni kuhakikisha Mzee Majuto anapata haki yake kwa kazi
mbalimbali alizofanya na kampuni hiyo.
"Mzee
Majuto alikwenda Mwanza na familia kupokea ule mzigo, meneja kwa
kumuheshimu akamfuata na kumwambia hiyo cheki hata senti tano hakuna na
cheki iliyobaundi ni kosa la jinai, tunachezea watu hivi.
"Mzee
Majuto ameacha familia yake, amekaa Mwanza zaidi ya miezi sita
anahangaika kuzipata hizo pesa, na mimi niko tayari nitatumia hata
mshahara wangu twende mahakamani tufunge watu tumeshachoka huko ni
kudharau watu" alisema Mwakyembe
Mwezi
Agosti Waziri Mwakyembe alimtembelea msanii nguli na mkongwe wa filamu
nchini Mzee Majuto nyumbani kwake ambapo alikwenda kumjulia hali baada
ya kupata taarifa kuwa anaumwa.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments