
Polisi huko Texas waliwaambia waandishi wa habari kuwa mwili huo
ulionekana kuwa wa Sherin ambaye habari za kutoweka kwake zilisambaa
mjini Dallas na India.
Wanandoa hao kutoka India walimpangisha mtoto huyo miaka miwli iliyopita kutoka makao ya kuwatunza watoto nchini India.
Polisi hata hivyo hawajatoa taarifa kuhusu ni kipi kilisababisha mtoto huyo aka fariki.
Mwili huo ulipatikana kwenye handaki kuribu nusu maili kutoka nyumbani kwao siku ya Jumamosi.
Baba wa mtoto huyo Wesley Mathews alikamatwa na kuachiliwa kwa
dhamana, kwa kuhatarisha maisha ya mtoto huyo baada ya kumfukuza kutoka
nyumbani usiku kutokana na sababu kuwa alikataa kumaliza maziwa
aliyokuwa akinywa.
Mama wa mtoto huyo inasemakana alikuwa amelala wakati mumewe alipokuwa amemtoa nje na kumfukuza mtoto wao.
Hata hivyo mtoto wao wa kwanza mwenye miaka minne teari amechukuliwa na serikali kwa ajili ya kumtunza kutokana na tukio hilo.
chanzo; zanzibar24.
Comments